Simanzi imetawala Aprili 06, 2023 wakati wa maziko ya aliyekuwa Mhandishi wa Wizara ya Maji, Hussein Chilala na mkewe, Furaha Rashid waliofariki dunia kwenye ajali iliyohusisha gari lao ndogo na treni katika makutano ya reli Kata ya Tambukareli jijini Dodoma. Maziko ya wanandoa hao yamefanyika katika Makaburi ya Sinza jijini Dar na kusababisha viunga mbalimbali vya Sinza kuzizima. Kwenye ajali hiyo ambayo waligonga kichwa cha treni wawili hao walikuwa na mtoto wao mmoja ambaye alitoka salama salimini!