
Dar es Salaam, 8 Aprili 2023: Wamiliki wa malori nchini kupitia chama chao cha TAMSTOA, leo wamezungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Double View iliyopo Sinza jijini na kuishuru serikali kwa kuwasapoti kwenye safari ya kwenda nchini Zambia na Congo DRC kufuatilia malori yao yaliyokwama kwenye foleni kwa zaidi ya miezi mitatu na changamoto zao nyingine nchini huko.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa TAMSTOA, Chuki Shaaban aliyeambatana na Katibu wa Chama hicho, Issa John na Mjumbe wa Kamati Mark Gama amesema baada ya kupata Baraka za serikali waliyafuatilia malori hayo nchini huko na kubaini dosari kadhaa ikiwemo wafanyakazi wa mipakani kwenye nchi hizo kufanyakazi kwa muda wa mchana peke yake na ikifika jioni wanafunga ofisi.

Chuki amesema wakiwa Zambia walipokelewa na balozi wa Tanzania ambaye wakiwa naye walishauriana na serikali za nchi hizo kufanyakazi masaa 24 ili kupunguza foleni hiyo na kuondoa kero hiyo kama zinavyofanya ofisi za mipaka ya nchi yetu ambazo zinafanyakazi masaa 24.
Jambo hilo limekubaliwa na nchi zote hizo Congo na Zambia kwa kutiliana saini ya makubaliano.
Uongozi wa TAMSTOA ukiwa nchini Zambia alibaini changamoto nyingine ya kuchelewesha malori yao kuwa ni ufinyu wa barabara unaosababisha foleni kubwa inapotokea dharura hata ndogo ya barabarani.

Changamoto walimfikishia Waziri wa Ujenzi wa Zambia, Chipoka Mlenda ambaye aliwaahidi kumaliza hilo kwa kuipanua barabara hiyo mara tu msimu wa mvua utakapomalizika.
Chuki amesema lengo lingine la mkutano huo ni kuiomba serikali iwapunguzie kodi ya uendeshaji wa shughuli zao kwani hivi karibuni imepanda kwa asilimia mia moja.
Mwenyekiti Chuki amesema ongezeko hilo la kodi limesababisha baadhi ya wamiliki wa malori kuyahamishia malori yao nchi jirani ambapo kodi zake za uendeshaji ni nafuu. Amesema Chuki na kuongeza;
“Tukiwa nchi hizo mbili tumekutana na magari kadhaa yaliyokuwa ya hapa nchini yamehamishia usajili wake kwenye nchi hizo jambo ambalo linatukosesha mapato.
“Tunamuomba Rais wetu, Mama Dk. Samia Suluhu Hassan aliangalie hili na kuzishauri mamlaka za kodi kutupunguzia mzigo huo sisi kama wafanyabiashara wazalendo tunaopenda kuichangia kodi serikali yetu na si kuhamishia biashara zetu nchi nyingine”.
“Chamoto nyingine kwenye umoja wetu tuliwaomba Latra madereva wetu kuingizwa kwenye mfumo wa kutambulika kimtandao (Data Base) ili rekodi zao zote ziweze kutambulika ili hata kama kuda dereva mwenye rekodi mbaya aweze kutambulika lakini mfumo huo umeonekana kuwa mgumu kupitia mfumo huo lakini hilo limekuwa gumu baada ya Latra kuwapa masharti magumu madereva hao kwa kuwaagiza kupeleka viambatanishi ambavyo wengi hawana”. Alimaliza kusema Mwenyekiti Chuki.
Chuki alivitaja baadhi ya viambata hivyo kuwa ni pamoja na vyeti vya kusomea udereva na vinginevyo. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL