×

Mshambuliaji Wa Simba Afunguka Mazito Baada ya Kupona Amtaja Baleke

Moses Phiri

MSHAMBULIAJI wa Simba, Moses Phiri amesema kuwa mara baada ya kupona kutoka katika majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua sasa anapambana kuona anapata nafasi na kuisadia Simba kufanya vyema katika michuano mbalimbali.

Phiri ameshindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya Simba mara kwa mara ambapo kocha Roberto Oliviera amekuwa akimtumia Jean Baleke katika eneo la ushambuliaji tofauti na yeye.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Phiri alisema: “Kila kitu ni mipango ya mwalimu kuhusiana na mimi kucheza au kutokucheza ndani ya Simba, naamini nitacheza tu.

“Unajua nilikuwa majeruhi kwa muda mrefu hivyo lazima nijipange vyema kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nacheza na naisaidia Simba kufanya vyema kwa kufunga mabao ya kutosha kama ilivyokuwa hapo awali.

“Ninafuraha kuwa Simba, ni timu kubwa ambayo ina malengo makubwa, ukiwa hapa mchezaji lazima uwe unawaza vitu vikubwa ili kuendana na Simba,” alisema mchezaji huyo.

Stori na Marco Mzumbe

“GOLI la MAYELE ni MCHEZAJI MKUBWA na MZOEFU, YANGA WALISTAHILI KUSHINDA”- UCHAMBUZI wa NGODA..

Leave a Comment