×

Kumbukumbu Ya Hayati Sokoine Kufanyikia Monduli Leo, Taasisi Sokoine Memorial Kuenzi Aliyoyaacha

Hayati Edward Moringe Sokoine.

12 Aprili 2023: Imekuwa ni kawaida ya binadamu kumsifia mtu anapotangulia mbelea za haki lakini hata hivyo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa na zaidi ya sifa za kawaida.

Kiongozi huyu anayetajwa kuwa wa mfano aliyepiga ulanguzi na unyonyaji kwa watu wa hali ya chini hata yeye mwenye hakupendezwa na maisha ya ufisadi kumbukumbu ya kifo chake inafanyika leo Inguiki, Monduli Juu mkoani Arusha Katika Kanisa Katoliki Monduli Juu.

Inaelezwa kuwa hata kifo chake kilichotokea tarehe kama ya leo kilisababishwa na uzalendo wake uliopitiliza wa kukataa kupanda helkopta aliyoandaliwa na kutumia msafara wa magari ili ajionee vizuri maisha ya wananchi ikiwemo kilimo kilivyokuwa kikiendelea pembezoni mwa barabara ambapo akaona angetumia helkopta huenda asingeona vizuri mashamba ya wananchi ikiwemo suala la kilimo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Hayati Edward Moringe Sokoine, Rembris Maranjus Kipuyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Hayati Edward Moringe Sokoine Rembrosi Maranjusi Kipuyo amesema kama ilivyo ada leo Aprili 12 wanafanya kumbukumbu ya miaka 39 tangu kifo cha Hayati Sokoine alipofariki dunia kwa ajali ya gari mkoani Morogoro.

Mwenyekiti huyo amesema katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa vyama na serikali na wazee wa kimila wameshathibitisha kushiriki ambapo pia wananchi wote wanakaribishwa.

Joseph Sokoine.

Rebrisi amesema lengo kubwa na kuanzisha taasisi hiyo ni kuenzi fikra, sera na misingi aliyoianzisha katika sekta y6a elimu, kilimo na mifugo lakini pia kuendeleza yale maono ambayo Edward Moringe Sokoine aliyokuwa ameyaacha.

Moja ya kazi kubwa ya taasisi hii ni kuhakikisha inaenzi fikra za Edward Moringe Sokoine ka kuziendeleza aliendelea kusema;

“Mfano katika ufugaji katika ufugaji alihakikisha tunakuwa na mifugo bora ambayo inampa mfugaji kipato na kiuchangia vyema pato la taifa na wafugaji wetu waachane na tabia ya kuhamahama kwa ajili ya kutafuta maji na malisho.

“Lingine taasisi hiyo imejikita kwa kuhakikisha wananchi wanajitosheleza kwa chakula na kuepukana na tabia bya kuwa ombaomba.

“Taasisi hii pia ikishirikiana na familia imejikita katika suala la mazingira kuhakikisha uhifadhi wa vyanzo vya maji.

“Wote tunakumbuka jinsi Hayati Sokoine alivyokuwa mzalendo na kulipenda taifa lake na wananchi kwa ujumla.” Alimaliza kusema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wa familia mtoto wa Hayati Moringe Sokoine aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Sokoine naye alitumia nafasi ya kuzungumza na wanahabari kuwakaribisha wananchi wote kwenye kumbukumbu hiyo ya miaka 39 ya kifo cha Hayati Sokoine.

“Naomba nitumie nafasi kuwakaribisha nyote kwenye ibada hiyo na baada ya hapo tutarudi nyumbani na kuendelea na shughuli ya kubariki kabuli la Hayati Sokoine”. Alimaliza kusema Joseph Sokoine.

KWA UFUPI HUYU NDIYE HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

Alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba 1980 tena akawa Waziri Mkuu kuanzia 24 February hadi tarehe  12 Aprili 1984.

Sokoine anatajwa kuwa mtu aliyepanda usawa kwa kila mtu aliamini kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika sekta mbalimbali ikiwemo ufugaji, kilimo na sehemu alipo na kujitegemea akiwa ni wakala wa mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu.

Alizaliwa Monduli mkoani Arusha Tanzania,  na kupata elimu ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958.

Mwaka 1961 alijiunga na Chama Cha TANU  baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962 mpaka hadi mwaka 1963.

Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo  la Masai.

Mwaka 1967 alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Usafiri na Kazi. Hatua nyingine katika maisha yake alijitangaza mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970.

Mwaka 1972 aliamia kwenye Waziri wa Usalama. Mwaka 1975 alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati huu kupitia Monduli.

Miaka miwili baadae akawa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Moja ya kazi kubwa aliyofanya kiongozi huyu ni kusimamia kazi kubwa ya kupambana na wahujumu uchumi ambapo serikali ya awamu ya kwanza iliamua kufanya oparesheni maalum ya kurudisha nidhamu kwa watumishi wa serikali pamoja na wananchi wengine huku waliojilimbikizia mali isivyohalali wakilengwa usimamizi ya oparesheni dhidi ya wahujumu uchumi ilijenga jina la Edward Moringe Sokoine.

Amebakia katika historia ya taifa la Tanzania huku akitajwa kama kiongozi aliyekuwa mchapakazi aliyeishi maisha ya wananchi wa kawaida na hakuwa mwenye ubinafsi ndio maana ilikuwa rahisi kwake kuwashughulikia viongozi wabinafsi na waliotumia vyeo kwa faida yao wenyewe.

Ndiye hasa aliyekuwa msimamiaji mkuu wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi na alifanikiwa kuweka nidhamu kwa watendaji na hakuwa na utani kwa watumishi wazembe.

Aliamini kuwa kila mwananchi mwenye afya njema anapaswa kujizalishia chakula chake mwenyewe na ziada kwaajili ya taifa na aliondoa dhana kuwa wajibu wa serikali si kumpatia mwananchi chakula.

Aliamini kuwa dhana ya kuitwa “mheshimiwa” ilikuwa kandamizi hivyo kumuita kiongozi mheshimiwa aliamini kuwa lazima kutakuwa na “mdharauliwa”.

MAKALA HAYA YAMEANDIKWA NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment