×

Bosi Simba Amkinga Kifua Sawadogo ni Mchezaji Mzuri

Ismael Sawadogo.

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuwa, licha ya kuonesha kiwango kisichoridhisha, Ismael Sawadogo, ni mchezaji mzuri ambaye anahitaji muda ili kurudisha kiwango chake.

Kiungo huyo aliyejiunga na Simba kipindi cha dirisha dogo msimu huu, ameonekana kutokuwa na nafasi kikosini hapo ambapo Jumatatu ya wiki hii, alitumia dakika 20 kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu, akaumia na kutoka uwanjani.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ally alisema: “Sawadogo ni mchezaji mzuri mwenye viwango japokuwa kwa sasa anapitia kipindi kigumu, lakini baada ya muda atakaa sawa na kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Maneno ni mengi kuhusu Sawadogo, lakini Klabu ya Simba bado tupo naye kuhakikisha tunamrejesha kwenye ubora wake, kwa sababu ni mchezaji ambaye tuna mkataba naye wa miaka miwili, hivyo bado ana muda mwingi sana ndani ya klabu.

“Naamini kuwa baada ya mchezo wetu dhidi ya Ihefu, Kocha Mkuu Robertinho (Roberto Oliveira) pamoja na msaidizi wake Juma Mgunda wanajua nini cha kufanya katika uwanja wa mazoezi ili kuimarisha kiwango cha fundi Sawadogo.”

YANGA KUISAMBARATISHA SIMBA, VIGOGO SIMBA SC WAMFUNGIA KAZI NABI… | KROSI DONGO

Leave a Comment