
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima leo Aprili 14, 2021 ameitambulisha rasmi Klabu ya Yanga kuwa mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Young Africans SC kuwa Mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto” amesema Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima
“Napenda kutoa rai kwa vilabu vya Simba SC, Azam FC, KMC na vingine vyote kuunga mkono kampeni hii, kampeni hii siyo mashindano ya kibiashara sote kwa pamoja tuungane na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kutokomeza changamoto hizi kubwa na kuilinda jamii yetu”
Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Klabu zetu ndio waathirika wakubwa wa hii vita dhidi ya ukatili wa kina mama na watoto, tusipowalinda kuna siku tutacheza mpira bila mashabiki Uwanjani”amesema Rais Hersi Ally Said
