×

Kikwete Apiga Simu Laivu Kenye Tuzo Za TMA, Atunukiwa Tuzo Ya Heshima -Video

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amepewa tuzo ya heshima na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) usiku wa kuamkia Aprili 30, 2023 kutokana na mchango wake katika tasnia ya sanaa.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kikwete amesema amefarijika kuona tasnia ya Sanaa Tanzania inaendelea vizuri kwa kupiga hatua kila siku.

“Napenda kuwashukuru wale wote waliotambua mchango wangu katika tasnia hii ya sanaa natumaini muziki wa Tanzania utaendelea kufika mbali,” amesema.

Leave a Comment