×

Prof Jay Aonekana Hadharani Anena ‘Hali Ilikuwa Mbaya, Nipo Imara’

MKONGWE wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Leonard Haule ‘Profesa Jay’amerudi tena kwenye mitandao ya kijamii kwa mara ya kwanza Mei 2, 2022 ikiwa ni baada ya siku zaidi ya 462 za kutokuweka chochote kwenye kurasa zake baada ya kuugua na kulazwa Hospitali ambapo kwenye post yake ameweka picha ya muonekano wake wa sasa.

Profesa Jay ameanza kwa kuandika “Salaam Ndugu zangu, kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu), pili kipekee namshukuru sana Mhe. Rais Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi, Asante sana Mama pamoja na Serikali yako yote kwani Viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji

Nitakuwa mchoyo wa Fadhila nisipoishukuru Familia yangu Mke wangu ( @Mke_wa_profjize ), kaka zangu, dada zangu Wadogo zangu na Familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mliomipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻”

ZAMARADI AFUNGUKA BAADA ya KUZINDUA TV YAKE – ”SIO KWAMBA NINA HELA, MUME WANGU HAKUNIACHA”…

Leave a Comment