Mkeka Wa Mbao Wazindua Bidhaa Mpya
August 2, 2024
0 Comments

Kampuni ya Classic Finishes Limited ambayo inafahamika zaidi kwa jina la Mkeka wa Mbao, imezindua bidhaa mpya ya Firmfit (sakafu) huku ikisisitiza bidhaa hiyo ni rafiki kwa uchumi na mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Classic Finishes Limited, Eda Sylvester amesema bidhaa zao zinazingatia ubora kulingana na wakati na hali za uchumi wa wananchi.
Pia Eda ameeleza kuwa kampuni ina uzoefu katika bidhaa za kupamba nyumba hususani kuta na sakafu na siku zote wanazingatia ubunifu na ubora wa bidhaa.
