×

Mabosi Simba Wampeleka Aishi Manula India Kupatiwa Matibabu

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula

IMEFAHAMIKA kuwa kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula muda wowote mabosi wa timu hiyo watamsafirisha kwenda nchini India kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu.

Kipa huyo anatarajiwa kurejea uwanjani katika msimu ujao kutokana na majeraha ya bega yaliyomsababishia aikose baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Akiwa anauguza majeraha hayo, nafasi yake ilikuwa inachukuliwa na kipa namba tatu wa timu hiyo, Ally Salim ambaye alionyesha kiwango bora katika Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika waliocheza dhidi ya Wyadd Casablanca ya Morocco.

Kwa mujibu wa mmoja wa mabosi kutoka Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, ameliambia Championi Jumatatu muda wowote kuanzia leo atasafiri kipa huyo kuelekea India kwa ajili ya matibabu.

Bosi huyo alisema kuwa, Manula akiwa huko India huenda akatumia wiki moja kwa ajili ya matibabu kabla ya kurejea nchini tayari kwa ajili ya kujiandaa na pre season.

Aliongeza kuwa hivi sasa wapo taratibu za mwisho za kukamilisha safari ya nchini huko tayari kwa ajili ya matibabu, licha ya uongozi upo katika mipango ya kumleta kipa mwingine atakayekuja kumpa changamoto.

“Manula muda wowote atasafiri kuelekea nchini India ambako atakaa kwa wiki moja kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya bega aliyoyapata akiwa majukumu ya timu.

“Lengo la kumpeleka huko India ili apone haraka kabla ya kuanza msimu mpya wa msimu ujao ambao tumepanga kuanza mapema.

“Tunafahamu umuhimu wa Manula, hiyo ndio sababu ya kupatiwa matibabu na uongozi, kwani aliumia katika timu, hivyo ni lazima timu imtibie,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally alisema: “Ni kweli Manula yupo katika matibabu, lakini hilo la kupelekwa India lipo kwa uongozi wa juu, taarifa lazima itatolewa.”

STORI: WILBERT MOLANDI

INJINIA HERSI ATINGA na MTOTO WAKE UWANJANI YANGA WAKITANGAZWA MABINGWA, ATOA KAULI HII….

Leave a Comment