×

Yanga: Tuna Dakika 180 Za Kazi Kimataifa Kutwaa Ubingwa CAF

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa, una dakika 180 za kazi kimataifa na watapambana kupata matokeo mazuri kufikia malengo ya kutwaa ubingwa.

Ni mbinu za Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia akishirikiana na msaidizi wake, Cedric Kaze, zinatarajiwa kutumika leo Jumapili ikiwa ni fainali ya kwanza Uwanja wa Mkapa, Dar dhidi ya USM Alger ya Algeria, kisha marudiano ni Juni 3, mwaka huu nchini Algeria.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema kwenye mechi za kimataifa wana kazi kubwa ya kufanya mechi zote mbili kutafuta ushindi ili kufikia malengo.

“Mechi mbili zote za kazi kimataifa ni muhimu kwetu kupata matokeo mazuri kwani kutwaa ubingwa ni lazima upate ushindi, haitokei kwa bahati mbaya.

“Ushirikiano ambao upo kwenye benchi la ufundi, wachezaji bila kusahau mashabiki ni nguvu kubwa kwa kila mmoja kuendelea kuwa kwenye mapambano na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Kamwe.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave a Comment