×

Papa Francis Asikitishwa na Ajali ya Treni India… Watu Zaidi ya 288 Wapoteza Maisha

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amesema amesikitishwa na ajali ya treni iliyotokea nchini India iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 288 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 900.
Papa alitoa salamu zake za rambirambi pamoja na maombi kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao.

Kadinali Mkuu wa Vatican Pietro Parolin, amesema kupitia Telegram kwamba Papa Franci pia amewaombea wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo na kuziombea pia juhudi za waokoaji za kuwatafuta manusura na miili zaidi.
Ajali hiyo ilitokea wakati treni ya abiria ilipoacha reli na kugongana na treni ya mizigo katika jimbo la Odisha nchini India.

RAIS SAMIA NDANI ya NDEGE MPYA, AKAA SITI ya RUBANI, CHEKI AKIITAZAMA MITAMBO KWA MAKINI…

 

Leave a Comment