×

Rais Samia Alivyozindua Ndege Mpya Ya Mizigo Aina Ya Boeing 767-300f Jijini Dar (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar,  Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuzindua Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023.
Rais Samia akiwa amekaa kwenye Chumba cha Marubani ya Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL mara baada ya kuizindua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023.
Rais  Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Mama Mariam Mwinyi mara baada ya kuzindua Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akishuka kwenye Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023


Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023

Rais  Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Marubani walioileta Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Captain Neema Swai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia akimpongeza mmoja wa Marubani walioileta Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Kapteni Neema Swai.
Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL ikiwasili na kumwagiwa maji watersalute mara baada ya kutua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023

Ndege mpya ya mizigo iliyonunuliwa na serikali, Boeing 767-300F iliyopewa jina la Air Tanzania Cargo ‘Lake Tanganyika’ imewasili salama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ikitokea nchini Marekani.

Kama ilivyo kawaida ya ndege mpya inapowasili, ndege hiyo imemwagiwa maji (water salutation) kuonesha heshima kwa kuwasili kwake salama na kugusa ardhi ya Tanzania kwa mara ya kwanza.

Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza mapokezi ya ndege hiyo ya kwanza ya mizigo kumilikiwa na serikali ambayo imerushwa na Kapteni Neema Swai.

Leave a Comment