
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi( UVCCM ) Wilaya ya Sengerema Mkoa Mwanza kimevuna Wanachama wapya 250 kwenye Kata ya Nyamatongo wakati ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye kata hiyo uliofanywa na kamati tekelezaji ya umoja huo.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Sengerema, Patrick Mundeba amewataka Wanachama wapya waliojiunga na umoja wajuone.kuwa wako mahali salama na sahihi kwao.

Patrick amesema yeye na Kamati tekelezaji watapitia kila Kata kutoa elimu na kuhamasisha vijana kujiunga na umoja ili chama cha Mapinduzi CCM kipate viongozi bora wa baadae kupitia ummoja huo.
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Sengerema amesema wataendelea kuunga mkono.jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Samia Suluhu Hasani za kuwaletea wananchi maendeleo.

Baadhi wa wanaCCM Kata ya Nyamatongo wameishukuru kamati tekelezaji ya UVCCM Wilaya Sengerema Kwa kuoan nivema kufanya ziara kwenye kata hiyo kwa lengo la kuona utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Kwa upande wake Katibu Hamasa wilaya ya Sengerema Ramadhani Janga amewataka vijina kuwa kuunganishwa nguvu na kuwa kitu kimoja Kwa lengo la kukitumia chama cha Mapinduzi.
