
Wasanii mbalimbali ni miongoni mwa wageni waliohudhurika katika kikao cha 41 cha mkutano wa 11 wa Bunge la 12 jijini Dodoma ambapo leo bunge linapokea na kujadili bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Wizara hiyo ambayo ndiyo inayowalea, inaongozwa na Waziri Dk. Pindi Chana huku naibu waziri wake akiwa hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’.

Miongoni mwa wasanii waliofika bungeni, ni pamoja na Mrisho Mpoto, Jackob Steven ‘JB”, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Bonny Mwaitege, Mc Pilipili, Yvonne Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ na wengine kibao.
