Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema “Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.4 kwa Mwaka 2023 kutoka Dola Bilioni 69.9 kwa Mwaka 2021.Tanzania sasa imepanda hadi nafasi ya sita ikilinganishwa na Nchi nyingize na Kusini mwa Jangwa la Sahara”
Kwa kutambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya Wananchi wanaishi Vijijini ambapo kilimo ndio msingi wa maisha yetu, Serikali iliongeza Bajeti ya Kilimo kutoka Tsh. Bilioni 294 kwa Mwaka 2021/2022 hadi Tsh. Bilioni 954 kwa Mwaka 2022/23 na sasa imeongeza hadi Tsh. Bilioni 970.8 kwa Mwaka wa Fedha 2023/24
Katika kuimarisha sekta ya kilimo, Serikali itaendelea kuongeza fedha kwenye sekta hiyo kadiri ufanisi utakavyoongezeka, hatua hii inaweza kuongeza fedha zaidi kwenye ya miradi ya Kilimo na kufika Tsh. Trilioni 1.27 katika Mwaka wa Fedha, tunataka kupiga vita kwa vitendo.