Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema ripoti ya Taasisi ya Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeonesha kuwa mpaka kufikia April, 2023, kulikuwa na miamala ya fedha haramu iliyofikia kiasi cha shilingi trilioni 280.
Mpina ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma na kueleza kuwa fedha hizo zimetakatishwa kupitia miamala mbalimbali inayofanwa nchini na hakuna jitihada zozote za serikali kukabiliana na suala hilo, jambo linaloikosesha serikali mapato na kuhatarisha usalama wa kiuchumi.