
Dar es Salaam, 26 Juni 2023: Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware amesema sababu kubwa inayochelewesha wadai fidia za malipo ni uchunguzi unaofanywa ili kubaini kama hakuna udanganyifu kwenye tukio husika na kuwaahidi wateja wa bima kufuatilia kiundani kama kutakuwa na sababu zinazosababishwa na wakala husika yeye kama yeye.

Nikiri kweli kuna mawakala wengine ambao wao kama wao wanafanya uzembe na kuwacheleweshea wateja kulipwa stahiki zao baada ya majanga hivyo naomba mteja yeyote anapobaini kuwa kuna uzembe kwa wakala anayemuhudumia atuletee malalamiko yake nasi tutayashughulikia mara moja.
Kamishna Dkt. Saqware alisema hayo kwenye mkutano mkuu wa mawakala wa bima nchini uliofanyika leo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mawakala kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mawakala wa bima ni wadau wetu wakubwa ambao wanatusaidia kazi kwa kiasi kikubwa sana ingawa kati yao kuna wengine ambao wanasababu za binanfsi zinazoweza kumcheleweshea mteja malipo yake. Alisema Kamishna Dkt. Saqware.
Akizungumzia mikataba ya bima kuandikwa kwa lugha ya kiingereza na kuwafanya wateja wengi kushindwa kuichambua vizuri amesema hilo linafanyiwa kazi na kufikia mwakani mikataba yote ya bima itakuwa lugha ya Kiswahili na kiingereza ili iweze kueleweka vizuri kwa wengi. Alimaliza kusema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Bima nchini, Sai John Daudi amesema makampuni ya bima yako machache kama 30 lakini sisi mawakala tuko wengi ambao tunafikia kama 1,200.

Mtu yeye anapochukua bima ni mkataba kati ya mteja na kampuni ya bima lakini kati ya kampuni ya bima na mteja tupo sisi mawakala wa bima ambao tunasaidia haya makampuni ya bima ambayo yanatuamini ndiyo maana hata kauli mbiu yetu inasema Uwakala ni Uaminifu hivyo nawasihi mawakala kuendeleza uaminifu huo ili tuwahudumie vizuri wateja wetu na kujenga taifa letu kwa ujumla. HABARI/PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL