
Aba Academy ni Watoto kuanzia umri wa miaka 3 mpaka 17 lengo kuu kukuza na kuendeleza Vipaji vya Watoto waliopo Mitaani, Majumbani, Mashuleni na katika Vituo maalumu vya kulea Watoto, hii ni kuunga mkono juhudi za Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kusapoti Michezo katik Taifa.
Akizungumza na Mtandao huu Pelham, amese ” Tunaomba sapoti ya Vifaa vya Michezo toka kwa Wadau Mbali Mbali ndani na nje ya Taifa, sapoti Michezo sapoti Watoto Taifa la leo ili tuwe na Timu ya Taifa tunaomba Serikali yetu, Wadau wa Michezo, Mashirika, Makampuni na Watu binafsi kuwekeza nguvu kwa Watoto kupata Vipaji na Wachezaji bora watakao tuwakilisha na kukupeperusha Bendera ya Taifa letu Duniani.

Mkurugenzi wa Aba Academy Sports Club amesema nia yake ni kuendelea kusaidia kukuza michezo nchini kwa kujenga msingi imara wa watoto katika soka la Tanzani ili kusadia kuandaa timu bora hapo baadae.
Pia amesema Shukrani za Pekee zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukuza soka la Tanzania katika michezo.
Aba amewaomba wadau na wapenzi wa soka kuiunga mkono timu hiyo kwa chochote kile watakachojaaliwa kwa kuchangaia mipira ya kutosha, Bips, jezi na viatu ili kudumisha soka kwa watoto kupitia namba ya simu 0785074040.
|
|