×

Muuaji Yanga Apewa Miaka Miwili Simba Try Again Afunguka

Mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis.

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis, ataendelea kuichezea timu hiyo, mara baada ya kufikia muafaka wa kuongeza mkataba wa miaka miwili.

Kibu alikuwa katika orodha ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu 2022/23, baada ya kujiunga na Simba msimu wa 2021/22 akitokea Mbeya City.

Kiungo huyo ndiye aliyefunga bao la pili katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata Simba dhidi ya Yanga katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara 2022/23.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, zinasema kwamba, sasa Kibu mkataba wake utamalizika Juni 2025 baada ya kuongeza miaka miwili.

Mtoa taarifa huyo alisema umuhimu na ubora wake Kibu ndiyo umewashawishi Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, kumuongezea mkataba huo.

“Hatuna mpango wa kumuachia mchezaji yeyote muhimu aliyekuwepo katika mipango ya timu kuelekea msimu ujao ambao tunakwenda kuandika historia katika michuano ya kimataifa.

“Tulichopanga ni kuwabakisha kwa kuwaboreshea mikataba yao ili tuendelea kubaki nao, huku tukiwaongeza wengine wapya watakaokuja kuifanya Simba imara.

“Kibu ni kati ya wachezaji ambao tuliowaongezea mikataba ya kuendelea kubaki Simba, kila mtu ameona kiwango cha mchezaji huyo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo la usajili, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alisema: “Hakuna mchezaji tegemeo atakayeondoka hapa Simba, kikubwa tutaendelea kuboresha mikataba ya wachezaji wetu.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

ALIYEKUWA MPIGAPICHA wa JUX AMWAGA SHOMBO kwa BOSI WAKE, ADAI MAKABILA KAMCHUKULIA MKE…

Leave a Comment