Charles Maige ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilimo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo.
Mwanafunzi anaeleza namna jambo hilo lilivyoanza ambapo anadai aliagizwa dukani na mwalimu huyo na baada ya kurudi mwalimu alimwambia aingie ndani na ndipo tukio hilo lilipotendeka kwa mara ya kwanza.
Aidha mwanafunzi huyo anaendelea kueleza kuwa akajenga mazoea ya kuwa ana mbakiza mwanafunzi huyo shuleni pindi wengine wanapoondoka na baada ya kukidhi haja zake alimtishia kwa kumfukuza shule au kumchoma kisu endapo atamueleza mtu yeyote.
Watu wengine kadhaa wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kile kinachodaiwa kufumbia mambo kitendo hicho cha kinyama.