×

Unga Unaoshukiwa Kuwa wa Cocaine Uliopatikana katika Ikulu ya Marekani Wazua wasi wasi

Kitu cheupe kilichosababisha uhamishaji wa dharura wa wafanyakazi katika Ikulu ya White House Jumapili usiku kilithibitishwa kuwa na cocaine.

Kitu hicho cheupe kilipatikana katika eneo la kazi wakati wa ukaguzi wa kawaida, Huduma za Siri za Marekani zilisema.

Rais Joe Biden na familia yake walikuwa mbali katika makazi ya Camp David wakati Cocaine hiyo hiyo ilipopatikana.

Jumba la White House lilifungwa kama tahadhari mwendo wa mbili na dakika 45 kwa saa za Marekani (01:45 BST) siku ya Jumapili baada ya maafisa wa huduma za ujasusi kupata unga mweupe “ndani ya eneo la kazi” la West Wing, msemaji wa Huduma za ujasusi Anthony Guglielmi aliambia BBC katika taarifa.

Bw Guglielmi alisema idara ya zima moto iliitwa haraka na kubaini kuwa mzigo huo “sio hatari”.

Alisema furushi hilo limetumwa kwa uchunguzi wa ziada na kwamba uchunguzi unaendelea, ikiwa ni pamoja na kubaini ni vipi mihadarati hiyo iliingia Ikulu.

#BREAKING: YANGA YAMTAMBULISHA NICKSON KIBABAGE, KUANZA na NYASSA BIG BULLETS ya MALAWI…

Leave a Comment