×

Wabunge SADC Wamuuunga Mkono Spika Tulia Kugombea nafasi ya Rais IPU

Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa pamoja wamekubaliana kumuunga Mkono Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Tulia Ackson, katika azma yake ya Kugombea nafasi ya Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani.

Jukwaa la Wabunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) limepitisha rasmi hoja kuhusu suala la dharura na umuhimu wa kikanda ili kumuuunga mkono mgombea wa nafasi ya Rais wa Umoja wa Wabunge (IPU),  Dkt Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania.

Hoja hiyo ilitolewa na Darren Bergman, Mbunge kutoka Afrika Kusini na kuungwa mkono na Pedro Senastiano Mbunge na mkuu wa Wajumbe kutoka Angola.

Dkt Tulia ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ni Rais wa Kundi la Kijiografia la Afrika ndani ya IPU, nafasi aliyokabidhiwa na wenzake kutoka nchi 53 za Afrika kwenye Mkutano wa 145 wa IPU uliofanyika Oktoba 2022 mjini Kigali, Rwanda.

Aidha Dkt Tulia ni wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye ana Shahada ya Uzamivu ya Sheria. Hakika kwa wasifu huu wa Dk. Tulia pamoja na rekodi yake ya utumishi katika nyanja za kitaifa, kikanda na Kimataifa zinajieleza zenyewe kwanini anastahili kuwa Rais wa ‘Inter-Parliamentary Union’

SIRI YAFICHUKA USAJILI wa MAYELE na UCHEZAJI BORA – BAMBO na ABBAS PIRA WAFUNGUKA….

Leave a Comment