×

Mbaroni kwa Tuhuma za Ubadhirifu Fedha za Maji

JESHI la Polisi mkoani Geita linawashikilia viongozi watatu wa kamati ya jumuiya ya maji inayosimamia mradi wa maji wa Mharamba uliopo wilayani Geita, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha wanazokusanya kwa wananchi kwa kuwauzia maji kwa kipindi cha miaka sita.

Viongozi hao walikamatwa mara baada ya kushindwa kujitetea juu ya matumizi ya fedha mbele ya Waziri wa Maji,Jumaa Aweso alipowauliza kuhusu kiasi kilichopo kwenye akiba ambacho kilitakiwa kuwa zaidi ya sh milioni 20 ndipo akaamua kuvunja kamati hiyo.

 

Baada ya Waziri kuvunja jumuiya hiyo Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Joseph Musukuma ameomba viongozi hao wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengine huku mkuu wa wilaya hiyo akiagiza kamati ya ulinzi kuwakamata kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Leave a Comment