
Dar es Salaam, 7 Julai 2023 – Takriban Maafisa Rasilimali na viongozi wa mashirika 200 walikutana katika Kongamano la People Managers Conference 2023 (#PMC23) lililofanyika tarehe 7 Julai 2023, katika ukumbi wa PSSSF jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulioandaliwa na Epvate na Fortune International Consulting (EFIC) ulikuwa na kauli mbiu “Usimamizi wa Matokeo Unaoweka Watu Mbele” ulidhaminiwa na NMB Bank.
Bi. Getrude Sima, alimwakilisha Mkurugenzi wa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) kwa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, kama mgeni rasmi.

“Leo, tumeshiriki majadiliano yanayohusu njia ambazo taasisi zinaweza kupata ukuaji huku ustawi wa waajiriwa ukiwa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa EFIC, Bwana Peter Mapigano. “Tulipata maoni mbalimbali kutoka sekta ya umma, taasisi binafsi, na waajiri, na yaliyochangia kuwa na kongamano lenye maongezi ya kina.”
Kongamano hilo lilileta pamoja wataalamu na wanataaluma walioelezea uzoefu wao kwenye maeneo tofauti, ikiwemo usaili wa wafanyakazi wenye vipaji, maendeleo na uongozi, ustawi wa wafanyakazi, ushirikishwaji, na masuala mengine yahusuyo kazi. Washiriki walipata ufahamu wa muhimu wa mikakati katika usimamizi wa rasilimali watu.

“PMC23 ilitoa fursa ya kutathmini umuhimu wa kuweka kipaumbele kwa watu kwenye kufanikisha malengo ya taasisi na kuleta mabadiliko chanya,” alisema Bw. Mapigano. “Tunajivunia kuwa tumetengeneza jukwaa lililowezesha kubadilishana maarifa, ushirikiano, na uvumbuzi katika usimamizi watu.”
Meneja wa Usawa wa Kijinsia na Ushirikishwaji wa ILO – Tanzania, Bi. Getrude Sima alisema ILO ilifurahia majadiliano haya yaliyokuwa na mvuto. “Watu ni kiini cha shughuli zetu ILO. Tulipata fursa ya kutoa uzoefu na mtazamo wetu kuhusu namna bora ya usimamizi wa watu,” alisema Bi Sima.
“Ni jambo linalotia moyo kuona wataalamu wa rasilimali watu na taasisi wakijadili kwa lengo la kuleta matokeo chanya,” alielezea Bi. Sima.

Bwana Mapigano alisema mkutano huu wa tatu wa PMC ulikuwa wa mafanikio yanayoonekana kupitia ushiriki wenye tija, mazungumzo ya kitaalamu, na fursa za kubadilishana maarifa . “Tulishuhudia idadi kubwa ya washiriki katika mkutano huu. Tunawashukuru washirika wetu NMB kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya.Uwepo wa watu kutoka sekta nyingine ulileta mawazo mapya,” aliongeza Bwana Mapigano.
Kwa Taarifa Zaidi: Fortunatus Ekklesiah
+255 745299676
Email : [email protected]