×

Fiston Mayele Afunguka Hatima Yake Yanga Ampa Onyo Fei Toto

Mkongomani Fiston Mayele

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mkongomani Fiston Mayele amesema kuwa Jumatatu ijayo itajulikana hatima yake ya kubaki ama kuondoka klabuni hapo mara baada ya kufanya kikao cha mwisho na uongozi wa timu hiyo, huku akimpa onyo swahiba wake, Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu, Fei Toto atambulishwe na Azam ilyompa mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo, kwa dau la Sh 200Mil.

Fei Toto ambaye ni rafiki wa karibu wa Mayele, tayari amejiunga na kambi ya Azam baada ya juzi kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwa safari ya kambi ya nchini Tunisia.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mayele alisema: “Hatima yangu ya kubakia au kuondoka Yanga, itajulikana rasmi Jumatatu ijayo baada ya kukutana na uongozi na kufanya kikao cha mwisho, ninaamini tutafikia muafaka mzuri wa kubakia hapa.

“Mimi nipo tayari kubakia hapa, kwani Wakongo wengi wanapenda hela, na mimi nimekuja hapa nchini kutafuta hela sio kitu kingine, kama ikitokea tukashindwana basi nitaondoka kwa amani kabisa bila ya kuwepo maneno maneno,” alisema Mayele.

Kuhusiana na Fei Toto kutua Azam, Mayele alisema kuwa Azam ni kati ya timu kubwa za kuogopwa kutokana na usajili ambao wanaoufanya katika kila msimu, lakini wanakosa makombe.

Aliongeza kuwa hilo tayari amemwambia Fei Toto, kwa kumtaka yeye awabadilishe na badala yake wacheze michezo yote katika kiwango bora bila ya kuangalia ukubwa wa timu wanayokwenda kukutana nayo.

“Juzi nilimwambia Fei Toto kuwa umekwenda kulekule ambako wenyewe wanakamia timu kubwa pekee za Simba na Yanga, lakini wanapokutana na timu ndogo wanapoteza.

“Azam ni timu bora yenye wachezaji wengi wakubwa ambao kwenye mechi kubwa wanacheza vizuri tena kwa kukamia, lakini wanapocheza na timu ndogo wanacheza katika viwango vidogo,” alisema Mayele.

Usiku wa kuamkia jana, Mayele alikuwa sehemu ya watu waliotangaza uzi mpya wa Yanga ambao rasmi ulizinduliwa huko nchini Malawi na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera sambamba na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said.

STORI NA WILBERT MOLANDI

NDEGE YA MIZIGO YA ATCL YAANZA SAFARI, YAENDA DUBAI NA SHEHENA KUBWA YA MIZIGO, RUBANI Azungumza…

Leave a Comment