×

TBL Yajitapa Kuimarika Licha Ya Kuwa Na Mazingira Magumu Ya Uzalishaji

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Lenard Mususa akizungumza kwenye mkutano huo.

Dar es salaam. Julai19, 2023. Kampuni ya bia (Tanzania Breweries Limited) imewasilisha mtazamo wa Bodi ya wakurugenzi kuhusu utendaji kazi wa Tanzania Breweries Plc kwa mwaka uliomalizika tarehe 31 Desemba 2022. Licha ya kuwepo kwa mazingira yenye changamoto kubwa, kampuni ilikuwa na ukuaji thabiti na ulioendelea kujenga thamani ya muda mrefu kwa wanahisa na wadau wengine hapa nchini Tanzania.

Mwaka uliopita ulikuwa mwaka mgumu wa aina yake duniani kote! Ulikuwa na changamoto za aina mbalimbali, zikiwemo mivutano ya tofauti za kisiasa za kimataifa (geopolitical tensions), vita nchini Ukraine,mfumuko wa bei uliokithiri na kuongezeka kwa viwango vya riba, vyote vikichangia katika kukifanya kiwe kipindi kigumu zaidi kwa muda mrefu.

Mkurugenzi wa TBL, Focus Lasway akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa bodi, Bw. Leornard Mususa alisema, “Mwaka 2022 ulikuwa na changamoto kubwa sana, lakini katika wakati huo ndipo nguvu na uimara halisi wa kampuni yetu ulijidhihirisha Ninajivunia dhamira na kujitoa kwa timu yetu katika kuleta matokeo bora. Pamoja, hatujapitia tu kipindi kigumu bali pia tumesimamisha msingi imara kwa ajili ya ukuaji wa baadaye.”

“Tunapata faraja kuwa tunawapa wateja wetu vinywaji vyenye ubora wahali ya juu, ambavyo vinawafanya waendelee kuvitumia. Katika mwaka 2022 tulishuhudia ukuaji mkubwa wa mapato, uliochochewa zaidi na ongezeko kubwa la mauzo ya bia” Anasema Bw. Mususa

Pamoja na hayo kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 la gawio hadi Tshs 85 bilioni (sawa na TShs 290 kwa kila hisa), ikilinganishwa na mwaka wa kifedha uliopita. Ukuaji huu wa gawio unaonesha dhamira thabiti ya kuongeza thamani ya kiuchumi kwa wanahisa.

Mwanahisa akiuliza swali kwenye mkutano huo.

TBL ni moja ya kampuni zinazoongoza kwa ulipaji wa kiwango kikubwa chakodi hapa nchini na pia ni mmoja wa wazalishaji na waajiri wakubwa. Lengo ni kuendelea kuwa raia wema. Katika mwaka huu uliopita, TBL ililipa jumla ya Tshs 528 bilioni kama kodi kwa serikali, ikilinganishwa na Tshs 472 bilioni zilizolipwa mwaka 2021. Pia TBL Imelenga kuwezesha watu, kwakuwa wao ndio rasilimali muhimu zaidi ya nchi hii na msingi wa ukuaji wote.

Mwenyekiti wa bodi, Bw. Leornard Mususa anasema “kwa kuwa tunapata karibu asilimia 74 ya malighafi zetu kutoka ndani yanchi, tumeweza kuchangia katika kuongeza ajira milioni moja,ukijumuisha za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Hii inaonyesha kwamba ahadi zetu sio maneno matupu. Tunatakakuwawezesha watu zaidi tukilenga kuunda mzunguko mzuri ambao ni endelevu.”

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Jose Moran akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Hata hivyo kwa Mwaka TBL imeanza mchakato wa kufungua kiwanda cha kuchakata shayiri, kilichopewa jina la Kilimanjaro Malting Plant, huko Moshi mkoa wa Kilimanjaro. Kiwanda hiki, ambacho kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi Machi 2024, kitaleta matokeo chanya katika sekta ya viwanda na uchumi wa ndani. Vile vile kitawezesha kuunga mkono zaidi juhudi za

Wanahisa wakifuatilia kiumakini mkutano huo.

serikali za kukuza sekta ya kilimo na kuboresha maisha ya wakulima,kwa kuongeza ununuzi wa shayiri wa ndani kutoka tani 5,000 hadi tani 12,000, na kisha tani 32,000 ndani ya miaka mitano.

Kuhusu Tanzania Breweries Limited

Tanzania Breweries Limited ni kampuni inayoongoza katika Sekta ya vinywaji nchini Tanzania, ikiwa na dhamira ya kuzalisha bidhaa bora na kuchochea ukuaji wa uchumi. Kama tanzu ya familia ya AB InBev, TBL inafanya kazi kwa kuzingatia wajibu mkubwa kwa wadau wake, ikijitahidi kuunda thamani na kuwa na athari chanya katika jamii.

Leave a Comment