Rais Hungary Awafungulia Watanzania Milango Nchini Mwake- (Picha +Video)
Global Publishers July 18, 2023 0 Comments
SHARE THIS:
Rais Samia akiwa na mgeni wake Rais wa Hungary, Katalin Novák wakati wakiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.
Rais wa Hungary, Katalin Novák amempa Rais Samia Suluhu mwaliko maalumu wa kuhudhuria kongamano maalumu la Budapest ambalo huwakutanisha viongozi mbalimbali wa kisiasa, kidini na wadau wengine mbalimbali ili kujadili suala zima la ongezeko la watu nchini humo.
Aidha, Rais wa Hungary, Katalin Novák amesema kwamba anawakaribisha watanzania wote kwenda kutembelea nchi yao kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo kusoma n ahata kuishi kutokana na uhaba wa rasilimali watu uliopo nchini kwao kufuatia sheria ambayo ilikuwa inawataka wananchi wan chi hiyo kutozaliana kwa wingi.
Rais Samia akizungumza na mgeni wake Rais wa Hungary Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Hungary, Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Hungary, Katalin Novák .Rais wa Hungary, Katalin Novák akiongoza ujumbe wa Nchi yake wakati wa mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai, 2023.Rais Samia akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Hungary ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo Katalin Novák, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe18 Julai, 2023.