×

#Exclusive: Kimewaka! Kumbuka Ajibu Tuhuma Za Kijana Aliyedaiwa Kumlawiti -Video

Kufuatia tuhuma za Kijana anayedai kufanyiwa ukatili wa kingono kwa kulawitiwa na mtangazaji na mshereheshaji mwenye jina lake hapa mjini, Dkt. Kumbuka, amefunguka na kuelezea jinsi ilivyokuwa na sivyo kama alivyoeleza kwenye mitandao ya kijamii kijana huyo.

Kumbuka ameelezea kuwa kijana huyo alimtafuta kwa lengo la kusaidiwa kiafya kwani alidai anaishi Kigoma, mara baada ya kukutana na kumbuka kwa lengo la kusaidiwa nyumbani kwake alianza kumpiga picha na kuchukua video kwa kila lililokuwa linaendelea nyumbani kwa Kumbuka.

Kumbuka anaeleza kuwa baada ya kumfuma akifanya yote hayo, kijana alisema yote kuwa ameagizwa na wala yeye haishi Kigoma kama alivyodai hapo awali bali alitumwa kumchafua na mtu aliseviwa kwenye simu kama Mshauri.

Kumbuka ameeleza kwa uchungu na kudai kuwa hana kinyongo na mtu ila anamuachia Mungu kwani kijana mwenyewe hakujua alitendalo.

Leave a Comment