×

Niger: Rais wa Niger aiomba Marekani msaada baada ya mapinduzi

Rais wa Niger aliyetimuliwa ameitaka Marekani na jumuiya nzima ya kimataifa kusaidia “kurejesha… utaratibu wa kikatiba” baada ya mapinduzi ya wiki iliyopita.

Katika maoni kwenye gazeti la Washington Post, Rais Mohamed Bazoum alisema alikuwa akiandika “kama mateka”.

Machafuko yamezuka katika taifa hilo la Afrika Magharibi tangu alipoondolewa madarakani.

Siku ya Alhamisi, viongozi hao wa mapinduzi walitangaza kuwa wanawaondoa mabalozi wa nchi hiyo kutoka Ufaransa, Marekani, Nigeria na Togo.

Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, walisema kazi za mabalozi wanne “zimekatishwa”.

Saa chache tu kabla, balozi wa Niger nchini Marekani, Kiari Liman-Tinguiri, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba wanajeshi “lazima wafikirie” na “kutambua kwamba jambo hili haliwezi kufanikiwa”.

Niger ni mzalishaji mkubwa wa uranium – mafuta ambayo ni muhimu kwa nishati ya nyuklia – na iko kwenye njia kuu ya uhamiaji kwenda Afrika Kaskazini na Mediterania.

Leave a Comment