

LEO Jumapili linafanyika Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali, kisha kikosi cha Simba SC kwa msimu wa 2023/24 kitatambulishwa rasmi, ikifuatiwa na mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Power Dynamos.
Kuelekea tamasha hilo, Wanasimba wameendelea kuwatambia wapinzani wao wakiwaambia: “Njooni muige, Simba raha tupu, sisi ndiyo wakali wa hizi kazi.”
Miongoni mwa viongozi waliofika kwenye tamasha hilo ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna ambaye aliambatana na viongozi wengine wa Benki hiyo tayari kwa ajili ya kushiriki burudani ya Simba Day!
Katika hatua nyingine Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye Tamasha hilo ‘Simba Day’ wamepata fursa ya kufunguliwa akaunti ya benki ya NMB kwenye banda lao lililopo Gate A. Akaunti hiyo ni maalum kwa ajili ya mashabiki wa Simba na zinakuja na ofa kibao!