Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Rehema Kamburuta almaarufu Mama Bocco, amesema anawaomba mashabiki wa simba kuanzia Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji, na mashabiki wengine wote kumsaidia ahame kwenye chumba kimoja anachoishi, Manzese Midizini jijini Dar es Salaam kwani haridhiki na mazingira anayoishi.