×

Rais Samia: Mashirika Ya Umma Yamekuwa Ni Sehemu Ya Kula Raha -(Picha + Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema mashirika ya umma yamekuwa ni sehemu ya kula raha na idadi kubwa ya watumishi wa serikali wamekuwa waking’ang’ania kuhamishiwa huko.

Rais Samia amesema wakurugenzi na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma, wanatakiwa kuhakikisha mashirika yao yanajiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa serikali.

Rais Samia ameyasema hayo katika ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha Agosti 19, 2023.

Viongozi na Watendaji wa Taasisi mbalimbali wakisikiliza na kufuatilia kwa makini Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Rais Samia akitoa Tuzo kwa baadhi ya Viongozi wa Taasisi na Kampuni zilizofanya vizuri kwenye kuchangia Maendeleo ya Serikali kwa Mwaka 2021/22, mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Rais Samia akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta maendeleo nchini , mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Rais Samia akitoa Tuzo kwa baadhi ya Viongozi wa Taasisi na Kampuni zilizofanya vizuri kwenye kuchangia Maendeleo ya Serikali kwa Mwaka 2021/22, mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Rais Samia akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023

Leave a Comment