
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa msanii wa kizazi kipya, Haitham Ghazal Seif amefariki dunia katika Hospitali
Taarifa za simanzi zilizotufikia hivi punde zinaeleza kwamba, aliyekuwa msanii maarufu wa kike wa
Bongo Fleva, Haitham Kim amefariki dunia.
Tangu wiki hii ilipoanza kulisambaa taarifa za kuumwa kwa Haitham ambapo mpenzi wake alithibitisha msanii huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.
Jana alhamisi taarifa hizo zilithibitishwa na kwamba alikuwa amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Hata hivyo, taarifa za hivi punde zilizothibitishwa na mmoja wa wa mameneja wa wasanii na mwandishi
wa nyimbo za Haitham aitwaye Ben zinaeleza kuwa mwanadada huyo amefariki dunia muda wa saa sita mchana katika Hospitali ya Temeke leo Septemba 1, 2023.
“Ni kweli Haitham amefariki dunia, ndiyo tupo hapa hospitalini kufanya taratibu za kuuhifadhi mwili.
“Kuhusu mazishi na taratibu za msiba naomba. unitafute baadaye,” amesema Ben Q.
Haitham ambaye anajulikana zaidi kwa Wimbo wake wa Fulani aliomshirikisha MwanaFA ameacha mtoto
Familia ya Global Digital inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa.
Pumzika kwa amani Haitham Kim🙏🏾