×

Vurugu za Gereza la Ekuador Walinzi Wachukuliwa Mateka

Zaidi ya walinzi 50 wa magereza na maafisa saba wa polisi wametekwa nyara katika jela kadhaa nchini Ecuador, kulingana na maafisa.

Mabomu mawili ya kutegwa ndani ya magari pia yaliyolipuka katika mji mkuu wa Quito, yote yakilenga mamlaka ya magereza nchini humo (SNAI).

Hakuna aliyejeruhiwa katika milipuko hiyo ya mabomu na takriban watu sita wamekamatwa.

“Tuna wasiwasi kuhusu usalama wa maafisa wetu,” alisema Bw Zapata.

Saa kadhaa mapema, bomu lililenga jengo ambalo hapo awali lilikuwa linatumiwa na SNAI huko Quito.

Polisi walisema shambulio hilo la baadaye lilitekelezwa kwa kutumia gari lililokuwa limetegwa vilipuzi.

Meya wa Quito Pabel Munoz alisema pia kulikuwa na milipuko ya guruneti katika jiji hilo wakati wa usiku.

Ecuador inakabiliwa na ongezeko la ghasia zinazohusishwa na magenge ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, ambayo yameweka matatizo makubwa katika mfumo wa magereza usio na rasilimali na msongamano mkubwa.

Mamia ya wafungwa wameuawa katika mapigano mabaya katika jela zilizojaa watu nchini Ecuador katika miaka ya hivi karibuni.

RAIS SAMIA-“MWAKANI KUNA KIVUMBI, MCHENGERWA NAMKUBALI SANA-NIMEMPELEKA TAMISEMI NAJUA ANAWEZA”

Leave a Comment