×

Rais wa Zanzibar Atengua Uteuzi wa Bosi wa Zanroads na Kamishna wa Idara ya Bajeti

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi leo Jumanne Septemba 12, 2023 ametengua uteuzi wa aliyekuwa Kamishna wa Idara ya Bajeti, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Saumu Khatibu Ally pia ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar (Zanroads), Makame Ali Makame.

Taarifa ya utenguzi hiyo imetolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said.

NECTA YATOA MAELEKEZO MAZITO kwa WANAFUNZI, WALIMU na WASIMAMIZI KUELEKEA MTIHANI DARASA la 7

Leave a Comment