×

Video: Necta Yatoa Maelekezo Mazito Kwa Wanafunzi, Walimu Na Wasimamizi Kuelekea Mtihani Darasa La 7 Septemba 13 na 14

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Said Ally Mohamed.

JUMLA ya watahiniwa 1, 397, 370 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika kesho Septemba 13 na 14 nchini kote.
Kati ya watahiniwa hao, 654,652 ni wavulana sawa na asilimia 46.85 na wasichana ni 742,718 sawa na asilimia 53.15.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Said Ally Mohamed ametumia fursa hiyo kuwataka watu wote wanaohusika na mitihani hiyo kuzingatia sheria na kujiepusha na aina zote za udanganyifu.

Dk Mohamed amesema kwa wanafunzi watakaobainika kufanya udanganyifu matokeo yake yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani na wahusika wengine watachukuliwa hatua za kwa mujibu wa sheria.

“Tunaamini wanafunzi wameandaliwa vyema katika kipindi chote cha miaka saba, hatutegemei kuona watahiniwa wanafanya udanganyifu kwa kuwa tutawafutia matokeo. Si kitu tunachokipenda kuona mtoto amesoma miaka saba halafu anafutiwa matokeo,” amesema Dk Mohamed.

CHOTA MAPENE ndiyo mchongo mpya town! Kwa shilingi 1,000 tu, yaani BUKU unajichotea mapene kibao au kupata nafasi ya kujishindia ZAWADI MBALIMBALI KILA SIKU, KILA WIKI kupitia Global TV, Global Radio na mitandao ya kijamii! ======================== Ingia kwenye simu yako📲, sehemu ya kufanyia malipo, andika namba ya kampuni 553111, kumbukumbu namba 255 au andika neno GLOBAL. Weka kiasi cha shilingi 1,000, weka namba yako ya siri, thibitisha na tuma.👍 PEASA UTATUMIWA MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO!🤝👍💰

Leave a Comment