×

Gamondi Awaonya Mastaa Yanga Kuvaana na Namungo Ligi Kuu Bara

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, raia wa Argentina, ameewaambia wachezaji wa timu hiyo akiwemo Kennedy Musonda kuwa hawana muda wa kubweteka wala kumpuuzia yeyote katika mechi zijazo.

Gamondi ametoa onyo hilo baada ya Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 0-2 ugenini dhidi ya Al Merrikh katika ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kufuzu hatua ya makundi.

Yanga ambayo inatarajiwa kurudiana na Al Merrikh Septemba 30, mwaka huu jijini Dar, kesho Jumatano inatarajiwa kuvaana na Namungo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema: “Tuna furaha kwa matokeo ya Rwanda, wachezaji walicheza vizuri, tumepata nafasi nyingine na kutumia mbili, lakini sasa tunaangalia mechi iliyopo mbele yetu kuhakikisha tunaendelea pale tulipoishia kwa kutafuta ushindi wa idadi kubwa ya mabao.

“Nimeongea na wachezaji kuhakikisha wanasahau matokeo ya mechi zote ambazo zimepita kwa sababu bado tuna jukumu kubwa na zito ambalo lipo mbele yetu, tuna mchezo mgumu Jumatano dhidi ya Namungo ambao tunahitaji kupata ushindi kabla ya kurejea kwenda Ligi ya Mabingwa katika mchezo wa marudiano, hivyo tunapaswa kushinda kila kitu bila ya kudharau mpinzani yeyote.”

STORI NA IBRAHIM MUSSA

ROBERTINHO MGUU nje NDANI, SIMBA WAMVUTA WINGA MZAMBIA/ YANGA SC YASUKA MIKAKATI MIPYA CAF..

Leave a Comment