
Benki ya Stanbic imezindua msaidizi wa kidigitali anaeweza kutoa huduma masaa 24, uzinduzi huu umefanyika Ijumaa, tarehe 22 Septemba.
Msaidizi huyu wa kidijitali ama chatbot atakuwa akitambulika kwa jina la Kai, inayolenga kubadilisha jinsi benki itakavyokuwa inatoa huduma za kibenki kwa wateja wake. Hatua hii inalenga kuleta suluhisho la kiubunifu na kukata kiu ya wateja katika kupata huduma bora zaidi. Uzinduzi huo ulifanyika kwa njia ya mtandao ambapo kongamano kuhusu maendeleo ya sekta ya kidigitali liliendelea katika hoteli ya Hyatt Regency mwishowa wiki.

Kai ni chatbot mwenye ufanisi, anayefungua ukurasa mpya wa namna wateja wanaweza kupata taarifa na usaidizi wa kibenki. Analeta urahisi na uharaka wa kupatikana kwa huduma na bidhaa za benki. Kai atatoa huduma kwa wateja masaa 24 na anapatikana kupitia WhatsApp namba +255 742 000 636 na kupitia tovuti ya Benki ya Stanbic Tanzania kwenye sehemu ya Chat.
Mkuu wa kitengo cha biashara wa Benki ya Stanbic Tanzania, Fredrick Max alisema, “Tunayofuraha kumtambulisha Kai, hii ni hatua kubwa ya maendeleo ya kidijitali.
Kai anaongeza kasi yetu ya kuhudumia wateja ikiwemo wa biashara ndogondogo na wakati. Tumejikita katika kukidhi mahitaji endelevu ya wateja wetu kwa kuhakikisha huduma za kibenki zinapatikana kwa urahisi lakini pia kwa ufanisi zaidi.”
Kai yupo sambamba na malengo ya kibiashara ya Benki ya Stanbic na yanayowalenga wateja kwani anaashiria hatua ya kimkakati kuelekea ufanisi zaidi na ufikivu katika huduma. Ubunifu huu sio tu unaboresha michakato ya ndani lakini pia unathibitisha kujitolea kwa benki katika kuwa mstari wa mbele katika teknolojia ya kibenki.
“Kwa wateja wetu muhimu, Kai anawakilisha hatua kubwa katika kuboresha huduma za kibenki. Tumejitolea kuwapa zana ya usaidizi wanaohitaji ili kuendesha shughuli zao za kifedha kwa urahisi. Utambulisho wa Kai unaturuhusu kukidhi mahitaji yao yanayoendelea, na kutoa njia ya haraka na rahisi zaidi ya kusimamia akaunti na miamala yao.” Aliongeza Max.
Mjadala uliokuwa na mada ya, Let’s Talk Digital iliyoendeshwa na Elvis Mushi, Mkurugenzi Mtendaji wa Redefine, ilitoa jukwaa kwa wadau wanaofahamika katika sekta ya kidijitali kujadili fursa na changamoto zinazokabili sekta ya uvumbuzi wa kidijitali nchini Tanzania.
Wanajopo ni pamoja na; Fredrick Max – Mkuu wa kitengo cha biashara katika Benki ya Stanbic, Edwin Bruno, Mkurugenzi Mtendaji/CVO – Smart Africa Group, Ian Usiri, Mkurugenzi Mtendaji – Ramani, Faith Pella, Mkuu wa Mikakati na Ukuaji – Kilimo Fresh, Nguvu Kommando, Mkurugenzi wa Huduma za Kidijitali – Vodacom Tanzania na Mihayo Wilmore, Makamu wa Rais, Mkakati – Airpay.