×

Director Kenny Alamba Dili Nono Infinix – Msikilize Afisa Uhusiano Akifunguka Mambo Ya Moto – Video

Huenda habari kuhusu Infinix ZERO 30 sio mpya masikioni mwako tangu kuzinduliwa kwake imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na blog za maswala ya tech.

Zero 30 inatajwa kuwa simu ya kwanza ulimwenguni kuja na selfie Camera ya Megapixel 50 yenye uwezo wa kurecord video kwa mfumo wa 4K 60fps kuuzika kwa gharama nafuu zaidi katika masoko ya simu.

kwa mujibu wa @infinixmobiletz simu hii kuja kuuzwa kwa kiasi cha bei za kitanzania Tsh. 1,060,000 tu katika maduka yote ya simu nchini.

Miongoni mwa mabadiliko ambayo yamefanywa katika toleo hili la ZERO kupitia ingizo la ZERO 30 ni pamoja na ongezeko la Refresh rate kutoka 120Hz hadi kufikia 144Hz.

Uzinduzi wa simu hii umefanyika  Septemba 26 ambapo Director Kenny @director_kennyy amepatiwa ubalozi na kampuni hiyo.
Kenny ameeleza kuwa safari yake ya kimaisha mpaka hapo alipofika alianzia kutumia simu hivyo vijana wasiogope kutumia simu katika kazi zao na amesisitiza kuwa siyo simu tu bali ni Infinix ZERO 30.

Pongezi nyingi sana kwa mabadiliko chanya kwa kampuni ya Infinix.

Leave a Comment