×

Mbunge Wa Arusha Mjini, Afunguka Miladi Mradi Wa TACTIC, Wadau Wapongeza – Video

Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema kuwa mradi wa TACTIC kwa jiji hilo tayari umeiva na mkandarasi ameshasaini mkataba kuanza kazi ya ujenzi wa barabara za jiji hilo kwa kiwango cha lami, ambazo zikikamilika zitabadilisha kabisa muonekano wa jiji hilo la Kitalii nchini.
Gambo amesema wakati anangumzia mradi wa TACTIC watu walikuwa hawaelewi ni kitu gani na walikuwa wanashangaa, lakini leo TACTIC imefika pazuri kiasi kwamba kila mwananchi anaweza kuizungumzia.
“Huu ni mradi maalum wa Serikali kwa ajili ya kuendeleza miji na majiji yetu. Katika halmashauri na majimbo yote yasiyopungua 180 nchi nzima, Serikali imeanza na majimbo 12 na miongoni mwa majimbo yatakayoanza kutekelezewa mradi huo ni Jimbo la Arusha Mjini. Mradi wa TACTIC Unakwenda kubadilisha kabisa sura ya Jiji la Arusha.
“Tayari mkandarasi ameshasaini mkataba wa kuanza kutekeleza mradi huo. Mradi utaenda kujenga
barabara za lami kuanzia maeneo matatu, barabara la lami ya Km 4.8 kwenye kata ya Sinoni (Barabara
ya Engoshelaton) mpaka Dampo la Murieti.
“Barabara ya lami kwenye raundi about ya Kwa Murombo kuelekea Golden City (Km 1.4) mpaka eneo ambalo itajengwa stendi mpya naya kisasa ya Arusha. Pia, lami kwenye barabara ya Olasiti inayoanzia Safina kwenda Kanisa Katoliki mpaka Mwisho wa Hiace na kutokea kwa Murombo (Km 3.96),” amesema Gambo.

Leave a Comment