×

Mpiga Solo wa East African Melody, Abdallah Bwiga Bwiga Afariki

Mpiga solo maarufu wa East African Melody, Abdallah Bwiga Bwiga, amefariki dunia.

Bwiga amefariki ghafla jana usiku na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa 7 mchana makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Jumatatu usiku, Bwiga aliyekuwa na uwezo pia wa kupiga bass gitaa, alishiriki vizuri onyesho la East African Melody ndani ya ukumbi wa Lango la Jiji.

Bwiga ameitumikia pia bendi ya Zanzibar Stars na hapo ndipo inasemekana alikuwa na historia ya kipekee.

Inasemekana Bwiga ndiye mpiga solo aliyerekodi nyimbo nyingi za Zanzibar Stars kuliko msanii mwingine yeyote yule.

Pamoja na hayo, Bwiga pia alikuwa mtu wa bendi zote, popote alipoitwa kwenda kusaidia show, hakusita kufanya hivyo pale nafasi inapomruhusu.

Watu wote wanakutana msikiti wa Mwinyimkuu Magomeni kuanzia muda huu.

Huu ni msiba mkubwa kwa tasnia ya taarab.

Stori na Said Mdoe

Leave a Comment