
Katika wiki ya AZAKI washiriki zaidi ya 500 kutoka asasi za kiraia, Serikalini na wadau wa maendeleo wanatarajiwa kushiriki katika wiki hiyo kwa mwaka huu 2023 ambayo inatarajiwa kuanza Oktoba 23 hadi 27 jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Oktoba 17, 2023 jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Bwana Francis Kiwanga amesema kongamano la mwaka huu litakuwa la kipekee kwani washiriki watapata fursa mbalimbali ikiwemo ya kukutana na wadau wa maendeleo na kuzungumzia masuala mazima ya teknolojia.
“Washiriki wa Wiki ya AZAKI watapata wasaa wa kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya taifa na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, serikali, wananchi, wanazuoni na sekta binafsi, kupitia kauli mbiu ambayo itakwenda kutumika kwa mwaka huu, teknolojia na jamii washiriki kufanya majadiliano kuangalia tulipotoka, tulipo sasa na tunapokwenda na kubadilishana mawazo, uzoefu na maarifa juu ya matumizi ya teknolojia kwa matokeo mazuri ya kijamii.

Katika masuala mazima ya teknolojia kwa hiyo itakuwa ni wiki muhimu sana hii, siyo wiki ya asasi peke yake bali ni wiki ya wananchi, kama mnavyofahamu asasi za kiraia zinafanya kazi karibu sana na wananchi wa Tanzania.
Kwahiyo nawasihi wananchi ambao hawajajisajiri waweze kujisajiri katika CSO wiki waje Arusha tuzungumze tufanye tafakari kubwa kuhusu sekta yetu ya AZAKI hapa nchini, ameeleza Bw. Kiwanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mlezi- Shirika la Malala, Bi.Nuria Mshare amesema katika Wiki Ya Azaki 2023 washiriki watapata wasaa pia wa kutajadili mchango wa teknolojia katika kuboresha elimu, majukwaa ya kujifunza kupitia mtandao na mafunzo ya walimu ili kuboresha matokeo ya ujifunzaji na kuziba mapengo ya kielimu.
“Mabadiliko ya kidigitali na kiteknolojia yamebadilisha mifumo yetu katika jamii kwa kiasi kikubwa na yana uwezo wa kuendelea kuleta mabadiliko mengine zaidi, mawasiliano juu ya makutano ya teknologia na jamii muhimu ili kuelewa mabadiliko haya kukabilina na changamoto zinazoleta katika jamii na kutumia fursa zinazotolewa.
“Katika wiki ya Azaki 2023 mada tofauti zitawasilishwa ikiwemo zitakazojikita katika kutathmini kauli mbiu ya Teknologia na Jamii, Ikiwemo; ujumuishi na uwezeshaji wa kidijitali na kutafakari kuhusu ujumuishi wa watu wenye ulemavu na matumizi ya teknolojia.”
Nae Bi.Doreen Dominic ambaye anawakilisha benki ya Stanbic amesema wameandaa namna ambavyo wataweza kushiriki ili waweze kuleta mabadiliko ya teknolojia kwa kuwa Sasa wamejikita kufanyakazi na asasi za kiraia ili iweze kutoa mchango wao kwa jamii.
“Tumekuwa karibu kushirikiana na baina na asasi tofauti tunakabiriwa na hamu kubwa ya kuchochea ushirikiano na ubunifu ili kuweza kuleta mabadiliko ya teknolojia.
Tunaelewa uwezo wa Teknolojia kwa duniani na tungependa tuwe na vyenzo mbalimbali vya kuwezesha hiyo teknolojia ifike hadi kwa jamii na tunashuru kwa kupewa nafasi hii kwa kushiriki na tunategemea tutafanya vizuri,” amesema Bi. Doreen.