×

Kihenzile Akagua Utekelezaji Maagizo ya Makamu wa Rais Tanga

Naibu waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amefanya ziara mkoani Tanga kukagua utekelezaji wa maagiza aliyoyatoa  Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango aliyoyatoa kwenye bandari ya Tanga.
Akiwa ziarani Tanga pamoja na kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na taasisi zilizo chini ya wizara ya uchukuzi, Kihenzile amesema Makamu wa Rais Dkt. philip Mpango aliagiza mambo matatu, kufungwa CCTV Camera katika bandari ya Tanga, Miundombinu ya reli kufika bandarini na kuhakikisha Magari ya Zimamoto yanakuwepo Badarini muda wote.
Kihenzile amesema ameridhishwa na utekelezaji wa maagizo hayo na kwamba kamera 49 zimekwisha fungwa katika bandari hiyo na kwamba suala la Ulinzi na Usalama wa Mizigo ya wateja katika Bandari ya Tanga linazingatiwa na hakuna tukio la kihalifu lililoripotiwa hadi sasa baada ya kuwapo kwa kamera hizo.
Ameongeza kuwa agizo la gari la zima moto  limeshaanza kutekelezwa na hivi sasa hatua inayofuata ni kusaini Mkataba (MoU) na pia bandari ya Tanga kwa sasa ina jumla ya  magari mawili ya zimamoto huku lile la kusogeza miundombinu ya reli bandarini Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  kwa kushirikiana na shirkia l Reli Tanzania (TRC) wameshakubaliana gharama za marekebisho, hatua inayofuata ni kusaini Mkataba (MoU

Leave a Comment