×

Makonda Aula Tena, Achaguliwa Kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo Oktoba 22, 2023 jijini Dodoma, imemteua Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.

Makonda anachukua nafasi ya Sophia Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Pia Halmashauri Kuu imemteua Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Leave a Comment