
Dar es Salaam 23 Oktoba 2023: Wamiliki wa malori nchini yaliyozuiliwa nchini Congo DRC kupitia Chama chao cha TAMSTOA wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuililia kupitia vyombo vya habari baada ya malori yao kushikiliwa nchini Congo DRC kwa zaidi ya siku hamsini na sasa kutolewa hati ya kuyarushu malori hayo kuendelea na shughuoli zake.
Akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Double View iliyopo Sinza jijini, Mwenyekiti TAMSTOA Chuki Shabani ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan baada ya kupata taarifa kutoka kwa madereva walioko nchini humo na malori hayo kuwa wamepata barua inayoelezea kuruhusiwa malori hayo kuendelea na shughuli zake.
Naye Katibu Mkuu wa TAMSTOA ameishukuru serikali kwa kuwasaidia kwenye changamoto zao kila zinapotokea ikiwemo sakata la kuzuiliwa malori yao yaliyobeba magogo kutoka nchini Zambia miezi kadhaa iliyopita ambapo waliiomba serikali iwasaidie nayo ikatoa msaada wa haraka na malori yao kuachiwa.
Sehemu ya barua ya kuyaruhusu malori hayo iliyoandikwa kwa lugha ya kifaransa.
