×

Halotel Yasherehekea Miaka 8

Mkurugenzi wa Biashara Halotel Bw. Abdallah Salum ( katikati ), akimkabidhi Mkuu wa shule ya Msingi Oysterbay Bw. Egidius Mjunangoma (kushoto katikati),moja kati ya Samani zilizotolewa kwa Shule hiyo ya Msingi Oysterbay Dar es Salaam kama ishara wakati wa tukio la kukabidhi vifaa hivyo leo kama moja ya msaada na muendelezo wa mkakati wa kuiboresha sekta ya elimu nchini kwa kuwapa mazingira bora Waalimu wakiwa ofisini ili kuongeza ufanisi wamaandalizi ya masomo kuwezesha kufundisha na wanafunzi kujifunza vema wakati Kampuni hiyo ikiendelea kuadhimisha miaka nane (08) ya kutoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini. Pamoja nao pichani ni baadhi ya  walimu na wanafunzi wa shule hiyo.

 

  • Yatoa Zawadi kwa Shule ya Msingi ya Oyster Bay

Dar es Salaam, 24 Oktoba 2023 – Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania inaadhimisha miaka 8 tangu kuanzishwa kwake hapa Tanzania kwa kuendelea kutoa kwa jamii na kukuza ubora wa elimu. Kwa ishara kubwa, Halotel inatoa viti na meza kwa walimu wa Shule ya Msingi ya Oysterbay kama sehemu ya jitihada za Kampuni katika Uwajibikaji kwa Kijamii. Mchango huu ni uthibitisho wa dhamira ya Halotel iliyojikita kwenye kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu nchini Tanzania, na lengo lake ni kuboresha mazingira ya kufundishia kwa walimu wa shule za Msingi.

Jitihada za Kampuni ya Halotel kwenye Kurudisha kwa jamii daima imejikita katika kuchangia kuboresha sekta ya elimu na nyinginezo nchini Tanzania. Kwa kutoa viti na meza bora kwa walimu, kampuni inalenga kutengeneza mazingira yanayofaa kwa ufundishaji wenye ufanisi, na hivyo kuathiri chanya uzoefu wa kujifunza wa wanafunzi.

Mchango muhimu wa Halotel unaendana na jitihada za serikali ya Tanzania kwenye kuongeza ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari. Serikali pia imejikita kwenye jukumu muhimu la kuwekeza kwenye uboreshaji wa mazingira bora ya kufundishia katika kuchochea utamaduni wa kujifunza na kupata mafanikio kwa wanafunzi. Mchango wa Halotel ni uthibitisho wa dhamira yake katika kusaidia jitihada hizi za serikali.

Katika hafla rasmi ya kukabidhi vifaa hivyo, wawakilishi wa Halotel, wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Biashara, walikusanyika katika Shule ya Sekondari ya Oysterbay kutoa viti na meza muhimu kwa walimu. Tukio hili lilikuwa ishara ya shukrani kwa jitihada na kazi muhimu ya walimu wote wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa tukio la makabidhiano katika Shule ya Msingi ya Oyster Bay, Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Bw. Abdallah Salum, alisema, “Tunapoendelea kuadhimisha miaka 8 ya Halotel, tunashukuru sana jamii ya Tanzania kwa mchango wao endelevu wa kutumia huduma zetu. Dhamira yetu ya Uwajibikaji wa Kampuni Kijamii unaendelea kuwa imara. Tunaaamini na kutambua kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya taifa letu, na kwa kuboresha mazingira ya kufundishia, tunaamini itawawezesha waalimu na wanafunzi kufikia uwezo wao kamili katika kufundisha na kujifunza.”

Kwa Upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi ya Oysterbay, Bw. Egidius Mjunangoma, alielezea shukrani na pongezi zake kwa msaada wa Kampuni ya Halotel. Alisema, “Tunashukuru sana Halotel kwa mchango wao mkubwa katika shule yetu. Viti na meza hizi za walimu zilizotolewa na Halotel zitaboresha sana mazingira ya walimu wetu ikiwa ni pamoja na ufundishaji katika shule yetu. Hatua hii ya ukarimu inaonesha dhamira ya Halotel katika kuboresha elimu, na tunapongeza kujitolea kwao katika kuleta athari chanya kwenye maisha ya wanafunzi na walimu wetu hapa shuleni. Ni faraja kubwa kuona sekta binafsi ikishiriki kikamilifu katika maendeleo ya mazingira yetu ya elimu, na tunatarajia jitihada za ushirikiano kama hizi zaidi hapo baadaye.”

Shule ya Msingi ya Oysterbay ni moja tu kati ya shule nyingi za Msingi na Sekondari katika sekta ya elimu zilizonufaika na jitihada za Uwajibikaji wa Kijamii wa Kampuni ya Halotel. Dhamira ya kampuni hii kwa elimu ni uthibitisho wa imani yake katika nguvu ya maarifa na dhamira yake ya kuboresha Sekta hii hapaTanzania.

 

Leave a Comment