×

Kuelekea Msimu Wa Sikukuu Tigo Yaja Na Mpango Wa Magifti Dabobado Zawadi Za Zaidi ya Mil 650 Kutolewa

Wahamasishaji wa Kamapeni ya Magifti Dabodabo (katikati) Hamisa Mobetto na Semaji la Kampeni hiyo, Haji Manara wakiwa na Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) na Mkuu wa Masoko wa Tigo, Edwardina Mgendi.

Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo leo imezindua kampeni ya Magifti dabobado ambayo inalenga kuwazawadia wateja wa Tigo ambapo mshindi atachojishindia atamchagua mpendwa wake naye kupewa zawadi kama hiyo buree, ndiyo maana ya mpango huo kuitwa Magifti dabodabo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha katika kampeni hiyo zawadi za zaidi milioni 650 kutolewa.

Angelica amesema miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na gari mpya kabisa aina ya Suzuki ambayo nayo inamwenzake kwa ajili ya kuzitoa dabodabo.

Kwa kusema hivyo amewataka wateja wa Tigo kuendelea kutumia huduma zao kwa kufanya miamala, kununua muda wa maongezi, vifurushi na huduma nyingine ili kuweza kuibuka mshindi.

Kampeni hiyo inanogeshwa na mwanamitindo Hamisa Mobetto pamoja na Semaji la kampeni hiyo Haji Manara ambao wote kwa pamoja wajihakikisha kuinogesha vyema kampeni hiyo.

Leave a Comment