
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania, Young Africans na Mabingwa wa kihistoria wa CAFCL, Al Ahly wametoshana nguvu kwa sare ya 1-1 katika dimba la Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
FT: YANGA SC 🇹🇿 1-1 🇪🇬 AL AHLY
⚽ Zouzoua 90+1’
⚽ Percy Tau 87’
Yanga SC imepata pointi ya kwanza kwenye hatua ya makundi CAFCL kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25.
MSIMAMO KUNDI D baada ya mechi mbili.
1. 🇪🇬 Al Ahly (4)
2. 🇬🇭 Medeama (3)
3. 🇩🇿 CR Belouizdad (3)
4. 🇹🇿 Yanga SC (1)