
Kampuni ya simu za Mkononi Airtel imeoneshwa kuguswa na tukio la waathirika wa wilaya ya Hanang na kuungana na watanzania wote kuwapa mkono wa pole waathirika.
Mkurugenzi wa Airtel bw, Dinesh Balsinghn amewaambia waliokumbwa na majanga hayo kuwa
‘Airtel tuko pamoja nanyi wakati huu mgumu ambapo Wilaya ya Hanang imekumbwa na maafaa. Tunatambua changamoto hii na tunatoa pole zetu za dhati’
Mkurugenzi wa Airtel ametangaza
Airtel kutoa dakika 100 za kupiga simu mitandao yote na GB 2 kuwasiliana na ndugu na rafiki kila siku kwa siku 3. Hii ni kwa lengo la kuendelea kurahisisha mawasilano kwa wateja wote wa Airtel waliopo eneo la tukio.
Mkuu huyo wa Airtel amebainisha kuwa Airtel itahakikisha kwa muda wote mawasiliano yanakuwa bora ili huduma za kijamii ziweze kuwa rahisi.